Simba SC Ijifunze kwa Vipers SC

Written by on February 10, 2023

” Kikubwa ni mabadiliko ya uendeshaji yaliyofanyika katika hii Klabu chini ya Mwasisi wa hii timu Laurence Mlindwa, moja kati ya Magwiji wa soka nchin Uganda ambaye amewahi kuwa Rais wa Chama cha soka Uganda FUFA kwa miaka 9 baada ya kumaliza akawekeza kwenye mpira”

” Mwekezaji ambaye anamiliki uwanja na Shule za St Mary’s , ametengeneza mfumo wa kuunganisha Shule pamoja na Academy za kuzalisha Wachezaji, amefanikiwa kuzalisha Vipaji vingi ambavyo vimeisaidia timu ya Taifa ya Uganda ambayo ina mafanikio makubwa ukanda wa CECAFA ”

” Vipers SC ni mfano kwa sisi hasa Simba ambaye wapo kundi moja kwenda kujifunza , ukipata nafasi kwenye Mashindano ya Kimataifa kuna vitu vingi unatakiwa kuvipata zaidi ya matokeo ya Uwanjani, kujua timu unayocheza nayo namna inavyoendeshwa , vitu vilivyofanya wafanikiwe kisha unaondoka navyo pamoja na matokeo yanakuja kukusaidia mbeleni”- @shaffihdauda_

WHEN DIGALA SPEAK , YOU HAVE TO LISTEN !!

@cloudssports
#HiliGame


Current track

Title

Artist