“Samatta Aheshimiwe”

Written by on January 22, 2024

Matokeo ya Taifa Stars katika michuano ya AFCON hayajawa ya kuridhisha mpaka sasa ikiwa imepoteza mchezo wa kwanza wa kundi E dhidi ya Morocco na kulazimishwa sare ya 1-1 na timu ya taifa ya Zambia ambayo ilikuwa ikicheza pungufu uwanjani. Lawama za baadhi ya mashabiki zimekuwa zikitupwa kwa wachezaji, akiwemo Mbwana Samatta ambaye ni nahodha wa kikosi cha Stars.

Hata hivyo mchambuzi wa michezo Farhan Kihamu kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X amemtetea Samatta na kutaka mashabiki wampe heshima anayostahili. Farhan amesema “Kuwa Captain na Staa wa nchi kama Mbwana Samatta kunakuja na gharama zake, yeye ni mwendelezo wa Mastaa wengi kwenye nchi zao ambao hubeba lawama hata kama hawastahili, game ya jana Captain kapika goli pekee, kafanya kazi kubwa mpaka kushuka chini kukaba ila bado watu watambebesha lawama, hii hutokana na ukubwa na mzigo ambao wakubwa hubebeshwa.

Haipo Tanzania tu bali duniani kote, utofauti tu ni kwamba watu wachache sana watakubali tuna Mbwana Samatta mmoja tu hatuna mwingine, pengine ndie Mchezaji wetu bora wa muda wote, ili afanye kile anachofanya Ulaya tunawahitaji Mbwana wengine wanne kila eneo, tunamtaka Mbwana wa Aston Villa, Genk, Paok ambaye hawezi kupatikana Tanzania.

All the best Captain Diego, real ones know the streets are watching”


Current track

Title

Artist