Yanga Imevuna Milioni 33 Kutoka kwa Viongozi

Written by on February 20, 2023

 

Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi Ally Said @caamil_88 amekiri kupokea Shilingi Milioni 15 kutoka kwa Mhe.Rais Samia Suluhu Hasaan, alizoahidi kununua magoli yatakayofungwa kwenye mchezo wao dhidi ya TP Mazembe , lakini pia Viongozi mbali mbali wameunga mkono kwa kununua kila goli moja kwa Milioni 1 na kufanya Jumla kuwa Milioni 33.

Viongozi waliotoa zawadi ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara , Waziri wa fedha , Waziri wa Sanaa na Michezo, Waziri wa Utalii , Naibu Waziri wa Ardhi, Mwenyekiti wa DRFA ( Hawa wote wametoa Milioni 1 kwa kila goli) fedha zote zitapokelewa na watapewa Wachezaji na Benchi la Ufundi amesema Rais wa Klabu ya Yanga kwenye LeoTena.


Current track

Title

Artist