Ukiuza Sukari Bei Juu Moshi Utayatimba

Written by on January 25, 2024

 

Bodi ya sukari Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limewakamata na kuwahoji Wafanyabiashara 18 kwa tuhuma za kuhodhi Sukari na kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya juu kinyume na bei elekezi ya Serikali.

Tarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi, Simon Msigwa imesema katika operesheni iliyofanyika Januari 22, 2024 kwa kushirikiana na Maafisa kutoka Bodi ya Sukari Tanzania watu 18 (Wanaume 13 na wanawake 5) wafanya biashara wasio waaminifu wa Moshi Manispaa walikamatwa kwa tuhuma za kuhodhi sukari na kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya juu.

“Uchunguzi ukikamilika hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mujibu wa kifungu na 11A cha sheria ya tasnia ya sukari No. 26 ya mwaka 2001 (sura ya 251) ya bodi ya Sukari Tanzania. “ ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

“Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linatoa rai kwa Wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali kuacha tabia ya kuhodhi bidhaa na kuuza kwa bei juu kinyume na taratibu, jambo linalozua taharuki kwa wananchi.” Iliongeza sehemu ya taarifa hiyo.

Kamanda Maigwa amewasihi pia Wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kuwafichua wafanyabiashara wasio waaminifu na wanaojihusisha na tabia hiyo ili hatua za kisheria zichukuliwe.


Current track

Title

Artist