MOTO WATEKETEZA KIWANDA CHA KUCHAKATA MBEGU ZA PAMBA

Written by on November 23, 2022

Shehena ya malighafi ikiwemo mbegu za pamba katika kiwanda cha kusindika na kuchakata mafuta ya kula cha Jielong kinachomilikuwa na raia wa China mkoani Shinyanga imeteketea kwa moto ambao chanzo chake bado hakijajulika usiku wa kuamkia leo.

Uhaba wa vifaa vya kukabiliana na majanga ya moto ikiwemo magari maalum katika mkoa wa Shinyanga yanatajwa kuchangia hasara kwa wamiliki wa nyumba na viwanda pindi wanapokumbwa na janga la moto na kusababisha wengi wao kupata hasara kubwa licha ya kutoa taarifa za majanga hayo kwa wakati.

Thomas Mayunga na Reuben Kitinya ni baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wanaelezea namna mto huo ulivyoanza. Kwa upande wake mkaguzi wa zao la Pamba kutoka bodi ya pamba Tanzania Thomas Daudi anaeleza hasara iliyojitokeza huku kaimu meneja wa kiwanda naye akieleza chanzo cha moto. Ramadhani Kamo ni mrakibu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Shinyanga ametoa tathmini ya awali ya madhara yaliyosababishwa na moto.


Current track

Title

Artist