ABC & Stallion wafanya muungano wa kutafuta suluhu na haki ya kisheria

Written by on February 17, 2024

Katika juhudi za kuunga mkono harakati za Mhe Rais Samia Suluhu za kupanua wigo na kuongeza fursa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya Tanzania, ndipo ambapo mawakili mahiri kutoka Tanzania wameamua kuunganisha nguvu na maarifa yao kutengeneza mwamvuli mmoja ambao utafanya kazi ya kupambania haki na mwisho wa siku kuleta maendeleo kwenye Taifa.

Muunganiko wa ABC Attorneys & Stallion Attorneys kuwa ‘Rive & Co’ unalenga kuongeza imani kwa wawekezaji wa kigeni kuja kuwekeza Tanzania kwani wengi huzingatia zaidi mazingira rafiki ya sheria zinazoweza kulinda haki zao na mali.

Akimuwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pindi Chana ndugu Hangi Chang’a ambaye ni Mkurungenzi Msaidizi wa Mashauri ya Katiba na Haki za Binadamu amesema:
“Huu ni muunganiko wa makampuni mawili ambayo kwa 100% ni za Watanzania lakini pia yanalengo la kudumisha Muungano kama mlivyosikia kuna mawakili kutoka Zanzibar na wamekuwa wakifanya shughuli za uwakili Zanzibar”

Pia ameongeza kuwa hii ni fursa kwa Watanzania wengi hasa mawakili kutoka mbalimbali kupata ajira na kujiendeleza.


Current track

Title

Artist