HAMA MJINI ULIPWE MILIONI 17 KWA KILA MTOTO

Written by on January 4, 2023

Serikali ya Japan itazipa familia hadi Shilingi milioni 17 (Yen 1,000,000) kwa kila mtoto kama zikikubali kuhama toka jiji la Tokyo kwenda sehemu nyingine.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyochapishwa katika mtandao wa Kyodo mpango huo unatajwa kuwa na lengo la kupunguza msongamano wa watu hasa wazee na kuhamasisha watu kuzaliana kutokana na Japan kutajwa kuwa na idadi kubwa ya wazee kwa mujibu wa Idara ya Takwimu ya nchi hiyo.

Watu wanaoishi vitongoji takribani 23 vya jiji la Tokyo wataweza kuomba mtonyo huo na watatakiwa kuishi nje ya Tokyo kwa angalau miaka mitano, endapo mhusika atavunja masharti hayo atatakiwa kuzirudisha fedha.

Vipi upewe shilingi ngapi uhame mjini?


Current track

Title

Artist