Sheria ya Kupiga Marufuku Mapenzi Kabla Ya Ndoa Yapitishwa

Written by on December 7, 2022

Bunge la Indonesia limepitisha sheria inayopiga marufuku raia au mgeni yeyote kujihusisha na mapenzi kabla ya ndoa. Sheria hiyo inazuia pia watu wasiokuwa wanandoa kuishi pamoja ambapo adhabu yake ni kifungo cha hadi mwaka mzima gerezani.

Baadhi ya makundi hasa ya vijana wameandamana kuipinga sheria hiyo itakayoanza kutumika baada ya miaka mitatu wakisema inaingilia haki za binadamu huku baadhi ya wamiliki wa biashara wakionya kwamba inaweza kufanya watalii na wawekezaji kuikimbia nchi hiyo.

 

 


Current track

Title

Artist