Sasa unaweza kufuta Ujumbe wa WhatsApp, ndani ya Masaa 60

Written by on August 10, 2022

Mwaka 2017, WhatsApp ilianza kuweka uwezo wa kufuta message ambayo umeituma. Mwanzo kabisa ilikuwa na limit ya Dakika 7; mtumiaji alikuwa na uwezo wa kufuta message ambayo ameituma, ndani ya dakika 7. Baada ya muda wa dakika 7 kuisha, mtumiaji alikuwa hawezi kufuta message ambayo ameituma. 

WhatsApp iliongeza muda wa kufuta message, kutoka Dakika 7 mpaka lisaa limoja, dakika 8 na sekunde 16. Kama unatumia toleo la zamani, hii ndio limit ambayo ilikwepo kwa watumiaji wengi. 

Katika Mabadiliko mapya, sasa watumiaji wote kwa sasa wanapewa muda wa Masaa 60 ya kufuta Message ambayo wamekosea kuituma au message ambayo unataka kuifuta. Ni sawa na Siku 2 na Masaa 12. 

Changamoto yake Hii ni kwa wale ambao wanatumia WhatsApp ambayo ni toleo jipya tu. Kama unatuma kwa mtu ambaye anatumia toleo la zamani, ujumbe utajifuta kwako tu lakini kwa mpokeaji utabaki.

Kama haujaona mabadiliko hayo, hakikisha unachukua toleo jipya katika App Store au Google Play. 

#CloudsTech 


Current track

Title

Artist