Niyonzima na Nyekundu ya Kujitakia kisa Simba

Written by on March 29, 2023

 

Mwamuzi wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania bara,Israel Mujuni Nkongo ameelezea moja ya tukio ambalo hawezi kulisahau la mchezaji kupanga kufanya mambo ya nje ya mchezo kwa Makusudi ili apate kadi nyekundu
.
“Ilikua kawaida yangu kuelekea mchezo fulani nilikuwa nafanya tafiti vijiweni, siku moja nikakutana na tetesi kuwa yupo mchezaji ambaye amepanga kuwa na matukio ambayo sio ya kawaida na anahusishwa kuihama Yanga kwenda Simba”

“Siku ya mchezo nyota huyo alicheza mchezo mbaya nikamuonyesha kadi ya njano,haikupita muda nilipuliza filimbi akaudunda mpira kwa hasira na kwa mujibu wa Sheria nilimuadhibu kwa kadi ya pili ya njano na kumtoa kwa nyekundu”

Inaendelea sehemu ya pili.

#CloudsDigitalUpdates
na @davidkampista .


Current track

Title

Artist