Mwamposa Alitaka Taifa Kufanya Maombezi

Written by on August 17, 2022

Mtume Boniface Mwamposa wa Inuka Uangaze Ameeleza kuwa Tanzania haina budi kuinuka na kuangaza kutokana na maombi ya kitaifa yatakayofanyika ijumaa tarehe 19-08-2022. Mtume Mwamposa ameyasema hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV.

Akiunga mkono maombi hayo yatakayojumuisha viongozi wa Dini zote amegusia kuwa maombi hayo ni muhimu kwa kuwa yataondoa giza katika taifa na kuleta nuru itakayoliangazia taifa katika mambo mbalimbali.

Ifahamike tu Tanzania imekuwa na utaratibu wa kuliombea taifa katika nyakati mbalimbali hata za kukabiliana majanga yanayolikumba taifa.

Ikumbukwe kuwa 2020 hayati John Pombe Magufuli alitangaza siku kadhaa za maombi ya kitaifa dhidi ya janga la UVIKO jambo lililosaidia taifa kupiga hatua katika mapambano ya janga hilo.


Current track

Title

Artist