Utata Kifo cha AKA na Mpenzi Wake

Written by on February 13, 2023

Rapper AKA, aitwaye Kiernan Jarryd Forbes, (35) alipigwa risasi na kufariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita nje ya mgahawa katika mji wa pwani wa Durban. Rapper huyo aliuawa pamoja na rafiki yake wa karibu, mpishi na mjasiriamali Tebello ‘Tibz’ Motsoane. Forbes amefariki ikiwa ni miaka miwili tu baada ya mchumba wake Anele ‘Nelli’ Tembe kufariki mwaka 2021. Tembe alijirusha kutoka ghorofa ya 10 ya Hoteli ya Pepperclub Jijini Cape Town.

Marehemu Anele ‘Nelli’ Tembe alikuwa mwanamitindo wa Afrika Kusini, mjasiriamali, na mtu maarufu kwenye mitandao ya kijamii. Alizaliwa Oktoba 11, 1999, katika familia tajiri huko Durban. Baba yake Moses Tembe ni mfanyabiashara mashuhuri na mwenyekiti wa Phumelela Gaming and Leisure Limited. Mama ambaye ni marehemu Lulu Msumi Tembe aliyefariki dunia mwaka 2004.

Katika mahojiano na Thando Thabethe, AKA alisema alikuwa kwenye mabishano makali na Nelli na wakati fulani katika mabishano yao alitishia kujiua mara kadhaa.

Rapa AKA ameacha Mtoto mmoja wa kike aitwaye Kairo Olwethu Forbes, aliyezaliwa mwaka 2015 aliyezaa na producer, Mtangazaji na DJ, aitwaye Ntombezinhle Jiyane (@djzinhle) (39).

#CloudsDigitalUpdates


Current track

Title

Artist