UWANJA WA TAIFA KUFANYA MATANGAZO KIDIGITALI

Written by on December 8, 2022

Serikali kupitia Wizara ya Michezo Sanaa na Utamaduni ikishirikiana na Kampuni ya kitanzania ya Formular 360 imeingia makubaliano ya kuweka Teknolojia ya kisasa ya matangazao ya Uwanjani kwenye Uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es Salaam  ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ubora wa Uwanja huo na kuongeza fursa ya upatikanaji wa kipato kwa Serikali yenyewe na Sekta Binafsi.

Hatua ya kufanyika kwa makubaliano hayo yenye thamani ya fedha za Kitanzania zaidi ya Shilingi Bilioni moja inatarajiwa kuwa Chachu ya kuongeza thamani ya Uwanja huo lakini pia kutoa  fursa kwa Taasisi na Mashirika mbambali kutangaza biashara zao kwa njia ya Kidigitali.

Akielezea Makubaliano hayo Mkurugenzi wa Miundombini kutoka Wizara ya Michezo Sanaa na Burudani ALEX MKENYENGE amesema kukamilika kwa Uwekezaji huo kutatoa fursa ya ukuaji wa biashara kwa wawekezani kutoka ndani na nje ya nchi.

 

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Clouds TV 🇹🇿 (@cloudstv)


Current track

Title

Artist