Harmonize Aomba Radhi Kwa Wimbo wa Bangi

Written by on December 8, 2022

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Clouds TV 🇹🇿 (@cloudstv)


Baada ya tamko la Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Gerald Kusaya, pamoja na kikao cha uongozi wa Konde Music Worldwide na Baraza la Sanaa la Taifa BASATA, uongozi wa Konde Gang umetoa barua ya kuomba radhi kutokana na wimbo wa ‘Weed Language’ wenye maudhui yanayokiuka utamaduni wa Tanzania.

Barua inaeleza -Uongozi wa konde music worldwide unaomba radhi kutokana na maudhui ya wimbo tulioutoa hivi karibuni unaoitwa ‘WEED LANGUAGE’:

Wimbo huu ulilenga kupanua na kukuza muziki wetu nje ya mipaka ya nchi yetu Lakini tafsiri ya maudhui ya wimbo huo yanakiuka maadili utamaduni, mila na desturi pamoja na miongozo ya mamlaka za serikali nchini Kutokana na kadhia iliyosababishwa na maudhui ya wimbo huo tunaomba radhi na tunahaidi kuuondoa wimbo huo kwenye mitandao yote ya kijamii.
Pia tunahaidi kuboresha nyimbo zetu ili ziendane na utamaduni wetu pamoja na miongozo ya mamlaka ya serikali.”


Current track

Title

Artist