Sam Sasali Aeleza Mambo Manne Yatakayomkuta Mchungaji Kimaro

Written by on January 18, 2023

Suala la Mchungaji Kimaro limekuwa na “Public Opinions” kwa sababu lina “Public Interest” pande mbili, wale wanamuunga mkono na Wale wasiomuunga Mkono na hii inatokana na Mchungaji Kimaro kuwa ni “Public Figure”.

Linapotokea Suala la Mpira kama lile la ‘Fei Toto” basi wataalam wa Soka wanakuwa na nafasi ya kutoa mawazo yao kwa wanavyoyajua mambo hata kama Jambo hilo sivyo hasa lilivyo. Linapofika suala la Kodi ama Tozo basi Wataalam wa Fedha na Mambo ya Uchumi wanakuwa na nafasi ya kutoa mawazo yao hata kama matokeo yatakuwa tofauti, vivyo hivyo katika kila Sekta. Wakati wa Corona tulifundishwa Kuwasikiliza “Wataalam” hata kama yale mawazo ya Wataalam hayakuwa sawa ila tuliwasikiliza.

Suala la Mchungaji Kimaro lina pande mbili, Upande wa Kwanza kuna Public Opinions ambazo zinaambatana na Upande mtu alioegemea. Kuna wanaosema Mchungaji Kimaro alikuwa na kiburi, alionywa mara kadhaa, kuna wanao tuma clip akiwasema madhehebu mengine, na kunwa wanaamini hili limekuja kwa sababu ya Kauli yake kuhusu Vijana wa kanisa Kutokuwa waamininifu kuliko wa kiislam na wengine wanasema Mchungaji Kimaro hafatishi Luturujia na Kalenda ya Kanisa hawa ni ule Upande unaomuhukumu moja kwa moja. Upande wa Pili ni Upande Unaoona Mchungaji Kimaro ameonewa, hata kama kweli amekosewa kwa Mchungaji kukaa Benchi siku 60 si ndogo huku wengine wakiamini ni “Church Politics” na “Ecclesiastical polity” Concept or approach haikufuata….Hapa kila mmoja anaweza kujimwagamwaga na kuandika cha kwake kwa ajili kutafuta “Public Sympathy” kwa Mchungaji Kimaro ama “Character Assassination” ya Mchungaji Kimaro Kuonesha kuwa hafai.

Nimesoma makala tofauti tofauti za watu akiwemo Malisa, akiwemo Baba Askofu Bagonza, alkini pia akiwemo Mwalimuwa Wangu Wakati wa Masomo ya Kiroho likiwemo “Romance Without Regreat” Baba Askofu Bandekile na wengine wengi. Ila wote pamoja na Mimi nadhani tunakosa Sababu hasa hasaaaa iliyopeleka kwa hiyo kila mtu anadondokea katika alichokisikia. Pengine kuna walioandika sababu hasa lakini hasa hasa iko moyoni mwa mtu.

Upande wa Pili ni Upande wa Kiroho ambao unapaswa kutazazwa na Watu Wa Kiroho na Kujikita katika hilo. Ukisoma kitabu cha Ufunuo wa Yohana 3:19-20 Utaona hakika Mungu huwa anawarudi wale awapendao. Inawezekana Mchungaji Kimaro akawa na Mapungufu kama binadamu sasa Mungu amechagua njia ya Kumsaidia kumponya kwa kumpitisha katika Pito hili kama Kuhani wa Bwana. Mbili Inawezekan Mungu anataka Kumuinua Mtumishi wake Mchungaji Kimaro lakini hawezi kwenda hatua kubwa Mpaka afaulu mtihani huu uliopo mbele yake kwa sasa, kama ambavyo huwezi kwenda darasa lingine mbele ama hatua kubwa ya kielimu bila mtihani vivyo hivyo kwa Mchungaji Kimaro.

Ukisoma Biblia Utaona Ili Yusufu awe Waziri Mkuu alipaswa kwanza Kupitia fedheha na changamoto ya kwenda Jela ndipo akavuka. Yesu Kristo kabla Hajakirimiwa Jina lipitalo Majina Yote ilimpasa kupitia aibu ya Mauti ya Msalaba. Hivyo basi Mtihani huu Mkubwa Mlengwa ni Mchungaji Kimaro either Mungu ana Mrudi ama Mungu anataka Kumuinua Sana. Ukitazama tarehe 17 Machi, 2023 haitakuwa Mbali saaana na tarehe 7 April, 2023 siku ya Ijumaa Kuu….Unaweza kuta hesabu za Mbinguni zimeshapigwa hapa.

Binafsi Sishangai Kuona Mchungaji Kimaro amepigwa Stop siku 60, nililiona likiwa linakuja na nina hakika hata yeye na watu waliokuwa karibu nae Watakuwa hawashangai kwa hili kuja labda litakuwa limewashangaza kuwa limekuja haraka sana pasipo wao kutarajia. Lilipoibuka Suala la “Youtube Account”, sijui School of Healing (wanaojua wanajua) Likaja Suiala la “Morning Glory” na evening Glory Wakati Uleee (Wanaojua wanajua), baadae tena likaja Suala la Vipindi katika Upendo Tv na mengine ambayo kwa sasa siwezi yaandika basi alipaswa akae mguu pande mguu sawa….Kwani siku hizi mnaona Clip za Mchungaji Mgogo ziki Trend??? Angejua tua Kinyozi Mwingine lakini Wembe uliomnyoa Mchungaji Mgogo nae angeanza tia maji kichwa ..Ya Mgisa Mtebe nitaandika Bwana akinijaalia.

Njia aliyochagu Mchungaji Kimaro ya Kutii Mamlaka ni njia bora zaidi kwa sasa ndani ya siku 60 na anapaswa kuwa Muangalifu na aulize kwa Uongozi kabisa kama anaweza Kuhubiri Youtube kama Mkristo mwingine yeyote anavyoweza hubiri youtube neno la Mungu, kwa maelezo ya Barua amezuiliwa kuwa Mchungaji lakini hajazuiliwa kuwa Mkristo au “Uchungaji”…Unaweza kuta hapaswi hata kumuombea mtu ama kuombea chakula ni vema akajua Mipaka ya Kusimamishwa kwake kabla hajakiuka pasipo kujua….

Zikifika siku 60 Mambo manne yatatokea. Hayahitaji Kujazwa na Roho ili kuyajua ila kwa akili tu ya Kawaida.

I. Mchungaji Kimaro atarejeshwa Kijitonyama Kwa Masharti (Iwapo Nguvu ya Umma Itashinda) Yeye akiwa sio wa Kwanza kutokea ndani ya Kanisa…

II. Mchungaji Kimaro akahamishiwa Usharika Mwingine…..Reference Case Mchungaji Mstai tokea Usharika wa Kunduchi

III. Mchungaji Kimaro Kupewa kazi nyingine katika Dayosisi au Nje ya Dayosisi, mfn. Mwalimu wa Chuo Cha Biblia, Kazi Maalum Makao Makuu…Ikimbukwe yeye haitakuwa mara ya Kwanza.

IV. Mchungaji Kimaro Kutoka KKKT na Kufanya huduma yake Mwenyewe…ikumbukwe yeye pia sio wa Kwanza hapa nchini.

Mchungaji Kimaro Ndani ya hizi siku 60 amlingane Bwana aliyemuita Kwenye Utumishi huu. Kila Jaribu Lina Mlango wa Kutokea.

Kama Paulo anavyomwambia anavyoandika katika Nyaraka zake kuwa anayo mengi ya Kuandika basi name ninayo mengi ya kuandika lakini kwa sasa wacha nikomee hapa Mpaka pale tarehe 17.


Current track

Title

Artist