Rose Ndauka Ajitoa Tuzo za Filamu

Written by on December 12, 2022

Wakati Bodi ya Filamu iko busy kutangaza Vipengele na Wanaowania tuzo mbalimbali kwenye vipengele hivyo katika Tuzo za Filamu mwaka huu, muigizaji Rose Ndauka (@iamrosendauka) ameandika waraka kuomba kujiondoa kwenye Tuzo hizo kwa kudai hastahili kuwania tuzo hizo kwa mwaka huu.

Rose ameandika -“NIMEKUWA KWENE TASNIA YA FILAMU ZAIDI YA MIAKA 14 SASA NIKIWA NA MILIKI TUZO MBILI KUBWA KAMA MSANII BORA WA KIKE 2011 ZIFF LAKINI PIA MWAKA 2013 MIN ZIFF, KIPINDI HICHO NILIKUWA NASTAHILI KUCHUKUA TUZO HIZO KWASABABU NILIKUWA WAMOTO 🔥🔥 NA NIPO KATIKA KIWANGO CHANGU BORA KABISA.”

“KULINGANA NA HILO KWASASA NAJIONA KABISA KISANAA NIMEFIKA KWENYE NAFASI SASA YA KUACHIA WENGINE HASA CHIPUKIZI WALIOFANYA VIZURI KATIKA KIPINDI HIKI CHA MIAKA MITATU NYUMA MPAKA SASA, KUNIWEKA KATIKA KIPENGELE CHA KUSHINDANIA MSANII BORA WA KIKE NA WASANII DAMU CHANGA WANAOFANYA VIZURI TENA KWA KUTUCHANGANYA NA WANAO ONEKANA MWAKA MZIMA NA SISI WENYE FILAMU YA LISAA LIMOJA MPAKA MASAA MAWILI KIUKWELI HAIKO SAWA 😔😔.”

“HIVYO BASI NAOMBA KUCHUKUA NAFASI HII KUISHUKURU 🙏 BODI YA FILAMU KWAKUONA NAFAA KUSHINDANIA KATIKA KIPENGELE HICHO NA KUNIWEKA,LAKINI BINAFSI NAOMBA KUBWAGA MANYANGA NA KUJIONDOA KATIKA TUZO HIZI ILI KUTOA NAFASI KWA WALE WALIOFANYA VIZURI NA WANAO STAHILI KUPATA HESHIMA HIYO,KULINGANA NA KWAMBA MIMI UKIANGALIA HAKUNA KAZI NILIYOIFANYA IKAWAFIKIA WATANZANIA KIPINDI HIKI CHA MIAKA MIWILI.”

Mtazamo wako ni hpi!? Share na sisi kwenye uwanja wa comments •


Current track

Title

Artist