Neymar Awashukuru Madaktari

Written by on December 6, 2022

Kwenye mahojiano na waandishi wa habari Neymar amewashukuru sana Madaktari kwa matibabu waliyompatia na kuhakikisha amepona kabisa hadi kuwa sehemu ya kikosi kilichoanza kwenye mchezo wa jana dhidi ya Korea Kusini.

“Nimecheza bila kuhisi maumivu yoyote , nawashukuru sana Madaktari kwa msaada wao na kunifanya kuwa sawa kwa mechi hii,nina furaha sana kwa kilichotokea usiku wa jana bila shaka nimecheza vizuri najua siwezi kuwa bora 100% ila nimetoa kilicho bora”- amesema Neymar


Current track

Title

Artist