Wazungu Wapanga Foleni ya Kuni

Written by on October 26, 2022

Wakazi wa kitongoji cha Glyfada kilichopo jiji la Athens nchini Ugiriki wamejitokeza kwa wingi kuchukua kuni za msaada toka kwa mamlaka ya jiji hilo ili kujiandaa na majira ya msimu wa baridi kutokana na kupanda kwa bei ya nishati ya gas.

Kuni hizo zimetokana na miti iliyoanguka wakati wa kimbunga kilichotokea mwezi Januari mwaka huu na kuhifadhiwa.

 

Asilimia kubwa ya wananchi wa Ugiriki wamejikuta katika hatari ya kushindwa kumudu gharama ya kuweza kununua nishati na chakula kutokana na mfumuko wa bei unaoendelea kuongezeka.

Ugiriki kama nchi nyingine za Bara la Ulaya zilikuwa zikiitegemea gas na mafuta kutoka Urusi hivyo kupelekea  mfumuko mkubwa wa gharama za nishati hizo kutokana na vikwazo vilivyowekwa kwa Urusi kuuza gas katika bara hili kutokana na vita inayoendelea baina yake na Ukraine.


Current track

Title

Artist