Musk Ameinunua Twitter Kwa Sh Trilioni 102

Written by on October 28, 2022

Baada ya miezi sita ya vuta nikuvute hatimaye Elon Musk amekuwa rasmi mmiliki wa mtandao wa Twitter. Musk amelipa kitita cha Shilingi trilioni 102.6 ambapo kila mwanahisa atalipwa Shilingi 126,373 kwa kila hisa moja anayomiliki.

Musk alionyesha nia ya kuinunua Twitter mwezi April mwaka huu kabla ya kubadili mawazo mwezi Mei akidai alidanganywa kuhusu idadi ya akaunti feki (bots) katika mtandao huo na kupelekea kampuni hiyo kumshtaki mahakamani. Hata hivyo kabla ya kesi kuanza kusikilizwa mwezi ujao Musk aliamua kuendelea na mpango wake wa awali.

Mara baada ya dili hilo kukamilishwa Musk amewafuta kazi Parag Agrawal aliekuwa Mkurugenzi Mtendaji, Ned Segal aliekuwa Afisa Fedha na Vijaya Gadde, Mkuu wa Sera wa kampuni hiyo.


Current track

Title

Artist