LIVE Updates: Moto Mlima Kilimanjaro

Written by on October 24, 2022

Na Dickson Busagaga

06:30: ZOEZI LA UZIMAJI MOTO KILIMANJARO LAINGIA SIKU YA PILI.

Baada ya siku ya Jana vikosi zaidi kupambana na udhibiti wa Moto katika Hifadhi ya Kilimanjaro zoezi Hilo limeingia siku ya pili kwa nguvu zaidi kuongezwa.

Viongozi mbalimbali siku ya Jana wamefika katika Hifadhi ya Kilimanjaro kwa ajili ya uratibu wa shughuli hiyo.

 

08:00 – JWTZ KUONGEZA NGUVU UZIMAJI MOTO

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Clouds TV 🇹🇿 (@cloudstv)

Zoezi linaloendelea la uzimaji Moto katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro tunaweza kusema “Hakuna kulala” Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof .Eliamani Sedoyeka anawasili usiku katika lango la Mwika kwa ajili ya kufafahamu maendeleo ya zoezi linaloendelea na baadae akazungumza na Clouds Digital akieleza suala la kuongeza nguvu.

 

13:15 – JAFO NA SEDOYEKA WAPANDA ENEO LILOUNGUA MOTO

WAZIRI wa Nchi ofisi ya Makamu wa rais Muungano na Mazingira Dkt Suleiman Jafo pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof Eliamani Sedoyeka wamepanda mlima kilimanjaro hadi mita 3100 kutoka usawa wa Bahari lengo likiwa ni kujiridhisha na athari zilizosababishwa na moto uliowaka siku tatu zilizopita katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Clouds TV 🇹🇿 (@cloudstv)

14:00 – MOTO MLIMA KILIMANJARO IFANYIKE TATHIMINI- JAFO

WAZIRI wa Nchi ofisi ya Makamu wa rais Muungano na Mazingira Dkt Suleiman Jafo ametaka kufanyike tathmini ya Moto Mlima Kilimanjaro wakati uchunguzi zaidi wa kina wa chanzo cha moto huo ukiendelea.

 


Current track

Title

Artist