SHAMRA SHAMRA MJENGONI MIAKA 20 YA CLOUDS

Leo Desemba 2, 2019 Redio Clouds FM imetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1999.

Mapema leo asubuhi kupitia kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV, Mkurugenzi wa Clouds Media Group alisema anawashukuru Watanzania kwa kuwa pamoja na redio kwa muda wote wa miaka 20.

‘’Leo ni siku ya kuwashukuru Watanzania ambao wametupa sisi heshima kubwa sana ya kuwa pamoja na sisi kwa kipindi chote cha miaka 20″ Alisema Joseph Kusaga.

“Maisha yote kila siku nasema nilifanya kitu cha kuwafungulia dunia watu, kuwafungulia maisha yao kuhakikisha maisha yao yanaendelea, Clouds ina miaka 20, maisha yangu ya biashara yana miaka 35” Aliongeza Joseph Kusaga

Tazama picha zaidi ilivyokuwa mjengoni leo.

Sakina Lyoka
Suzy Bartazary

0 Reviews

Write a Review

Leave a comment