Nandy ni ndugu yangu- Billnass

Msanii wa Bongo Fleva, William Nicolaus Lyimo ‘Billnass’ amevunja ukimy baada ya tetesi kusambaa kwa muda mrefu kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake wa muziki huo, Faustina Charles Mfinanga, “Nandy”.

Amesema hayo kwenye mahojiano kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM wakati ngoma yake ya Bugana iliposimama kama Jiwe La Wiki.

“Kiukweli mimi na Nandy tulifanya kazi kama ambavyo watu wanaona, na kazi ilifanya vizuri, uhusiano wetu baada ya kazi tumekuwa kama ndugu” Alisema Billnass

Pia msanii huyo amezungumzia ujio wa ngoma yake mpya kuelekea kilele cha Tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika Desemba 8, 2019 kwenye uwanja wa Uhuru, Temeke jijini Dar es Salaam.

“Kwa kuwa tunaelekea kwenye sikukuu ya kitaifa kiburudani tarehe 8 Dec naona kuna haja ya kuwaongezea mashabiki wangu ngoma mpya, kuanzia sasa tegemeeni chochote kuelekea kilele cha Tigo Fiesta” Aliongeza Billnass.

0 Reviews

Write a Review

Leave a comment