Nafsi inanisuta kumtetea Rosa Ree- Mwana FA.

Baada ya msanii  wa Bongo Fleva, Rosary Roberts ‘RosaRee’ kufungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kutojihusisha na muziki kwa miezi 6, kutokana na kuvuka kwa video zake za ngono, Staa wa muziki huo, Hamis Mwinjuma amesema nafsi yake inamsuta kumtetea msanii huyo.

Amezungumza hayo leo Jumamosi, Novemba 30, 2019 katika kipindi maalum cha Bongo Fleva, ‘Round Table’ cha Clouds FM.

“Rosa Ree ni mdogo wangu lakini nafsi yangu itanisuta kama ntaenda kumtetea kutokana na video yake, nafkiri hata yeye hadhani kama ameonewa, me nafikiri tumuache atumikie adhabu yake” Alisema MwanaFA.

“Ingekuwa amri yangu hakuna msanii yeyote ambaye angefungiwa, lakini siwezi kuingilia maamuzi ya Basata, na ninahusiwa sana niweze kuwaachia watendaji waweze kutenda kazi yao” Aliongeza MwanaFA

0 Reviews

Write a Review

Leave a comment