Mtoto anayesomeshwa na Program ya NdondoCup amaliza masomo ya awali, afaulu.


Mtoto Mohamed Rashid Ramadhan ambaye anasomeshwa na project ya Ndondo Cup chini ya Clouds FM amemaliza masomo yake ya awali na kuwa miangoni mwa wanafunzi waliofanya vizuri na mwakani anaanza darasa la kwanza.


Muddy anasomeshwa katika shule ya Msingi Tusiime iliyopo jijini Dar es Salaam, baada ya kushinda tuzo ya shabiki bora na kuchaguliwa kuwa balozi ya mashindano hayo mwaka 2017.
Muddy alikuwa anakwenda na baba yake uwanjani kwenye mashindano ya Ndondo Cup akiwa amenyolewa kwa ‘style’ mbalimbali huku akiwa amevalishwa mavazi ya kuvutia hususani ya asili ya Kimasai.
Jana Jumamosi Novemba 31, 2019 ilikuwa mahafali ya 21 ya shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo.

0 Reviews

Write a Review

Leave a comment