MIAKA 20 STUDIO TATU

Ikiwa leo Desemba 2, 2019 Clouds FM imetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, redio hiyo imehama studio tatu tofauti katika ofisi yake ya makao makuu iliyopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Hivi karibuni redio hiyo imehamia kwenye studio mpya lakini kabla ya hapo, ilikuwa kwenye studio mbili tofauti katika ofisi za makao makuu ya redio hiyo iliyopo Mikocheni.

Mkuu wa Idara ya Ufundi, Clouds Media Group, Jackson Joseph ameelezea sababu ya kuhama kwa studio. Amezungumza alipokuwa akihojiwa na kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv.

“Nadhani mliona mazingira ya studio B, zamani ndio ilikuwa studio inayokwenda hewani, nafasi yake ilikuwa ni ndogo, kipindi kile tulianza na chumba kidogo kutokana na uwezo tuliokuwa nao, baada ya kukua kidogo tukaona sasa tujitanue tukahamia kwenye studio kubwa ambayo ilikuwa imeboreshwa na kubwa zaidi kama inavyoonekana lakini hii ina tofauti na ile mpya inayotumika sasa hivi” Alisema Jackson.

“Teknolojia inabadilika kila wakati hii studio mfumo wake ni ‘analogy’ tumeingia kwenye mfumo mpya, sasa hivi redio nyingi zinahama kutoka kwenye mfumo wa utangazaji wa ‘analogy’ kwenye digital” Aliongeza Jackson

0 Reviews

Write a Review

Leave a comment