FIESTA ILILETA WASANII WAKUBWA WENYE VIWANGO DUNIANI- KUSAGA

Mkurugenzi wa Clouds media Group, Joseph Kusaga amesema Clouds Media Group ilileta wasanii wakubwa wa Kimataifa kwa ajili ya kupafomu kwenye jukwaa la Tigo Fiesta.

Amezungumza hayo leo Jumatatu Desemba 2, 2019 katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 ya Redio Clouds.

“Tulishawaleta sana, wasanii wakubwa wa viwango vya Dunia. Tunashukuru walikuwa na mchago kuwafanya wasanii wetu wajifunze machache kutoka kwao, wengine tuliwatengenezea nafasi za kufanya Collabo na wasanii wetu ikawa mwanzo wao kutoka Kimataifa” Alisema Joseph Kusaga

“Tigo Fiesta itaendelea kuwa jukwaa la wasanii wa Tanzania pekee. Wao wanatosha na hilo ni jukwaa lao kuonesha ukomavu. Wasanii wa nje tunaweza kuwaalika katika shoo nyingine lakini Fiesta ni 100 Tanzania” Aliongeza Joseph Kusaga

Joseph kusaga ameonesha picha za baadhi ya wakali wa Kimataifa waliowahi kupafomu kwenye jukwaa la Fiesta baadhi yao ni T.I, Lil Kim.

0 Reviews

Write a Review

Leave a comment