Asilimia 34% ya Watanzania wana Bima ya Afya.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bernard Konga amesema asilimia 34 ya Watanzania pekee ndio wako kwenye mfumo wa Bima ya Afya.

Ameyasema hayo leo Jumapili Desemba 1, 2019 alipokuwa akihojiwa kupitia kipindi cha Njia Panda cha Clouds FM.
“Asilimia 34 pekee ya Watanzania ndio wako kwenye mfumo wa Bima, ina maana huyu Mtanzania akiugua magonjwa ya muda mrefu wakati hana Bima ndio mwanzo wa kiingia kwenye umasikini” Alisema Bernard Konga

“Kama nchi ajenda yetu imejikita kwenye masuala ya Bima, kwa sababu ni kitu ambacho kitamwezesha mwananchi kupata matibabu yake pindi anapoumwa bila ya kupata kikwazo chochote au kuingia kwenye umasikini” Aliongeza Bernard Konga.

0 Reviews

Write a Review

Leave a comment