Kwenye treni, kipaumbele cha kwanza ni usalama- Mkurugenzi TRC

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Nchini, (TRC) Masanja Kadogosa amesema kipaumbele cha kwanza kwenye usafiri wa treni ni usalama wa abiria na mali zao wakiwa ndani ya treni.

Amezungumza hayo leo Ijumaa, Desemba 20, 2019 kwenye mahojiano maalum kupitia kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV.

“Usalama kwenye Treni ni Kipaumbele chetu cha kwanza, usalama ndani ya treni yetu ni mkubwa sana kwani kuna Kikosi cha Polisi cha reli ambacho kinahakikisha usalama wa Treni pamoja na Abiria na mali zao, hivyo hakuna sababu ya Watu kuhofia usalama wao katika safari za treni”. Masanja Kadogosa, Mkurugenzi Mkuu, TRC.

Aidha akizungumzia idadi kubwa ya abiria katika mikoa inayotegemea sana usafiri huo alisema “Bado tunakabiliwa na Idadi kubwa ya abiria hasa katika maeneo ambayo usafiri wa treni ndio unaotegemewa sana, mfano Mpanda na Kigoma. Hivyo wakati mwingine abiria wanalazimika kusimama kutokana na hali halisi ya uhitaji wa usafiri, pamoja na sisi kuwa na nia ya kutaka kuwahudumia”.

 
 

Leave a comment