Hawa hapa watoto wa Freeman Mbowe

Written by on December 19, 2019

Sio rahisi kuwaona watoto wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) kwenye mikutano mbalimbali ya chama hicho, lakini imekuwa tofauti kwenye mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika jana Jumatano Desemba 18, 2019 katika ukumbi wa Mlimani City, Mwenge, jijini Dar es Salaam.

Watoto hao watatu ambao walitambulishwa na baba yao, walikuwa kati ya wageni waalikwa katika mkutano huo.

Katika mkutano huo pia ulifanyika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho ambapo Freeman Mbowe alipata ushindi wa asilimia 93.5. kwa kupata kura 886 akimshinda mgombea mwenzake Cecil Mwambe aliyepata kura 59 pekee sawa na asilimia 6.2 huku kura 3 zikitajwa kuharibika.

 

Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist

Background