Wawili waongezewa Mkataba Azam, Ndikumana atupiwa vilago

WINGA machachari, Idd Kipagwile ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu ya Azam FC, mabingwa wa Kombe la Shiriksho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Kipagwile anayesifika kwa mashuti, kuchachafya mabeki na kasi yake uwanjani, atabakia kutoa huduma yake ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2022.

Huyo anakuwa mchezaji wa pili kuongeza mkataba ndani ya kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo, baada ya kipa Mwadini Ally aliyeongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Mkataba wake pia amesaini jana Jumanne, Desemba 18, 2019 mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, utamfanya Mwadini kusalia kwa wababe hao kutoka Azam Complex hadi Julai 2021.

Leave a comment