FREEMAN MBOWE MWENYEKITI mpya CHADEMA, TUNDU LISSU MAKAMU.

Freeman Mbowe amefanikiwa kutetea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo Taifa kwa kupata ushindi wa asilimia 93.5. Mbowe aliyepata kura 886 amemshinda Cecil Mwambe aliyepata kura 59 pekee sawa na asilimia 6.2 huku kura 3 zikitajwa kuharibika.

Tundu Lissu ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara) baada ya kupata kura 930 sawa na 98.8% akimshinda Sophia Mwakagenda (aliyetangaza kujitoa akiwa ukumbini) aliyepata kura 11 sawa na 1.2%.

Said Issa Mohamedi ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Zanzibar) nafasi ambayo ilikuwa na mgombea mmoja pekee.

Uchaguzi huo umefanyika usiku wa kuamkia leo Jumatano, Desemba 18, 2019 katika ukumbi wa Mlimani City uliopo Mwenge Mwenge jijini Dar es Salaam.

Leave a comment