Tuzo za Malkia wa Nguvu ni mwanga kwangu- Latifa

Mshindi wa tuzo ya Malkia wa Nguvu 2017, kupitia kipengele cha biashara, Latifa Mohammed amesema tuzo hiyo imempa mwanga na kuweza kumfungulia milango mbalimbali katika biashara zake.

Amesema hayo leo Jumanne Desemba 17, 2019 kupitia kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv.

“Baada ya kupata tuzo ya Malkia wa Nguvu, iliweza kunifungulia milango mingi sana, na watu wakishakuona wanaanza kukuamini na kukufuatilia unachokifanya, niliweza kuongeza hata ‘product’ nilizokuwa nazifanya, Malkia wa Nguvu ilikuwa ni mwanga kwangu” Alisema Latifa Mohammed, ambaye pia ni Mkurugenzi Shirika la Wezesha Binti na Mama Mjasiriamali.

“Nilifanya vitu vingi hasa kwenye kampuni yangu ya Queentipha Products tunakuwa na ‘product’ mbalimbali kama kisamvu, ‘popcorn’ na vitu vingine lakini zaidi nimeweza kufungua taasisi yangu ambayo inaitwa Shirika la Wezesha Binti na Mama Mjasiriamali ambayo ilianzishwa mwaka mwezi wa saba, ina Lengo kubwa la kuweza kuwainua kimaisha na kiuchumi wanawake na mabinti wa Kitanzania” Aliongeza Latifa Mohammed.

Leave a comment